Home Soka Mashujaa Fc Yavuta Wawili Kigoma

Mashujaa Fc Yavuta Wawili Kigoma

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Mashujaa Fc imekamilisha usajili wa wachezaji wawili beki wa kati Carlos Protas akitokea Biashara United ya mkoani Mara sambamba na aliekua mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Sc Mohamed Mussa ambapo tayari wameshatambulishwa rasmi.

Mashujaa Fc yenye makazi yake mkoani Kigoma inaboresha kikosi chake baada ya kuondokewa na mastaa kadhaa ambapo Musa anakuja kuziba pengo la Reliant Lusajo ambaye amejiunga na klabu ya Dodoma Jiji Fc huku Carlos akisajili kuziba nafasi ya Samson Madeleke ambaye amejiunga na Pamba Jiji Fc ya jijini Mwanza.

Tayari mpaka sasa mastaa hao wametambulishwa rasmi katika mitandao ya kijamii ya klabu hiyo kama wachezaji wapya klabuni hapo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu nchini.

banner

Mashujaa Fc ilipanda daraja na kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu nchini msimu ulioisha ambapo ilifanikiwa kumaliza katika nafasi ya nane ya msimamo ikiwa na alama 35 baada ya kucheza michezo 30 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited