Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili kusalia klabuni hapo kiungo wake Adolph Mtasingwa Bitegeko ambaye alikua anamaliza mkataba wake Januari mwakani.
Awali tetesi zilisema kuwa kiungo huyo alishamalizana na klabu ya Yanga sc kwa kukubaliana kila kitu ambapo ilikua ikisubiriwa amalize mkataba wake ili atue jangwani.
Leo mapema klabu hiyo ya Azam Fc imethibitisha kumuongezea mkataba mpya ambapo atadumu klabuni hapo mpaka mwaka 2027 huku usajili huo ukimfurahisha kocha Yousouph Dabo wa klabu hiyo kutokana na bado alikua na mahitaji na kiungo huyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mtasingwa alikulia katika akademia ya Azam Fc kisha mwaka 2019 alijiunga na KR Reykjavik ya nchini Iceland na baadae alijiunga na klabu ya Koflavik kisha akarejea KR Reykjavik kisha akajiunga na Volsungur na baadae alirejea Azam Fc msimu wa 2023 mwezi January.