Home Soka Ateba Atua Simba Sc

Ateba Atua Simba Sc

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba Sc imekamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Cameroon Lionel Ateba kutoka klabu ya Usm Algers inayoshiriki ligi kuu nchini Algeria kwa mkataba wa miaka miwili.

Awali mshambuliaji huyo alihusishwa na Yanga Sc lakini baadae alijiunga na miamba hiyo ya soka nchini Algeria ambapo Simba sc imelazimika kununua mkataba wake uliosalia klabuni hapo ambapo takribani milioni mia saba zimetumika kukamilisha usajili huo.

Ateba anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo akishirikiana na Steven Mukwala ambaye bado hajamridhisha kocha Fadlu Davis katika michezo michache aliyoshiriki mpaka sasa.

banner

Ateba pamoja na kutarajiwa kufanya makubwa nchini Algeria bado hakua na takwimu za kushtua ambapo katika michezo takribani 23 alifunga mabao matatu na kutoa usaidizi wa upatikanaji wa mabao mengine saba.

Kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo moja kwa moja kunamuondoa kipa Ayoub Lakred kikosini humo ili kukidhi idadi ya wachezaji 12 wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited