Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kiluvya United katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex siku ya Septemba 4.
Yanga sc imecheza mchezo huo ikiwa ni kujiandaa na michuano ya ligi kuu na kuwaweka fiti mastaa wake ambao hawajaitwa katika vikosi vya timu zao za Taifa.
Mastaa waliokuwepo vikosini humo kwa upande wa Yanga sc walimaliza mchezo huo kwa ushindi wa mabao hayo matatu yaliyofungwa na Jean Baleke,Salum Abubakari na Shekhan Khamis ambaye pia anakwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Vijana ya miaka 20 ambayo itaingia kambini Kigamboni Dar es salaam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha Miguel Gamondi anawaandaa mastaa waliobaki kikosini ili kuwaweka sawa na mchezo dhidi ya CBE ya Ethiopia utakaofanyika Septemba 14 nchini Ethiopia na kurudiana baada ya wiki moja jijini Dar es Salaam.