Kocha wa klabu ya Simba Sc Fadlu Davis amesema kuwa mastaa Yusuph Kagoma na Abdulrazak Hamza wanatarajiwa kuukosa mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Kmc kutokana na kuwa na majeraha.
Fadlu amesema hayo mapema hii leo ikiwa ni katika mkutano na waandishi wa habari kama ilivyo utaratibu wa bodi ya ligi ambapo kila timu huzungumza waandishi siku moja kabla ya mchezo.
Mchezo huo utakaofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo Fadlu Davis amesema kuwa atawakosa mastaa hao kutokana na kuwa katika matibabu ya majeraha yao.
“Kagoma na Valentino Mashaka bado wanakosekana ila Abdurazak Hamza ameanza mazoezi na wenzake japo hayupo tayari, pia hayupo kwenye mipango ya mchezo wa kesho dhidi ya KMC FC. Amesema Kocha Fadlu Davids.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia mshambuliajiwaklabuhiyoStephen Mukwala amesema kuwa wao kama wachezaji wanacheza kwa kujitoa kupambania nembo ya klabu hiyo.
“Tunacheza kwa kujitolea kwasababu ya nembo ya Simba SC halafu jina langu litakumbukwa baadae ila kwanza unajituma kwa ajili ya nembo ya Simba ndio maana sisi wachezaji hatukati tamaa hadi mwisho”. Alisema staa huyo aliyefunga bao la ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa Fc .
Simba sc endapo itashinda mchezo huo itafikisha alama 25 na kuipiku Yanga sc ambayo ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini ikiwa na alama 24.