Timu ya As Vita ya nchini Kongo iliyokua ije nchini kumenyana na Yanga sc katika siku ya kilele cha tamasha la wiki ya mwananchi imeahirisha kuja nchini kucheza na wanajangwani hao kama ilivyoelezwa hapo awali.
Roul Shungu ambaye ni kocha msaidizi wa timu hiyo amethibitisha kuahirishwa kwa safari hiyo ya kuja nchini baada ya kutangazwa kwa ratiba ya michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika ambapo timu hiyo itaanzia ugenini nchini Cameroon dhidi ya UMS de Loum.
Kwa mujibu wa ratiba ya tamasha hilo ilibidi timu hizo zimenyane Agusti 4 ambayo ndio siku ya kilele na timu hiyo ya Kongo ingebakiwa siku tano za maandalizi na kusafiri kwenda Cameroon kitu ambacho wakongo hao wameona ni vigumu ukizingatia umuhimu wa michuano hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia kocha huyo amesisitiza ratiba hiyo ya Caf licha ya kuathiri ushiriki wao katika tamasha la wiki ya mwananchii pia itawalazimu kubadili ratiba yao ya maandalizi ya msimu ili kujiandaa na mechi hiyo.