Home Soka Kamusoko Aibukia kwa Lwandamina

Kamusoko Aibukia kwa Lwandamina

by Sports Leo
0 comments

Thabani Skala Kamusoko kiungo fundi mwenye Rasta aliyeinogesha ile staili ya kampa kampa tena hatimaye amesajiliwa na klabu ya Zesco Fc ya Zambia inayonolewa na kocha wa zamani ya klabu ya Yanga sc George Lwandamina.

Kiungo huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea Fc Platnum na Power Dynamos za nchini Zimbabwe alitemwa na wanajangwani baada ya mkataba wake kuisha kwa kigezo cha umri na majeruhi baada ya ya ripoti ya kocha Mwinyi Zahera kuonyesha kutomuhitaji kiungo huyo.

banner

Kamusoko amesaini mkataba wa miaka mitatu kukipiga Zesco  na hii inachangiwa na kiwango alichokionesha katika michuano ya Afcon hasa katika mechi dhidi ya Uganda ambayo iliisha kwa Sare ya magoli moja kwa moja.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited