Uongozi wa Timu ya Kmc Fc umemfuta kazi kocha Kali Ongala kutokana na baadhi ya changamoto zake ndani ya timu hiyo yenye makao yake makuu katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Tayari Kali Ongala amefutwa kazi hiyo jumamosi ya mei 03 2025 na hayupo na timu kuanzia muda huo japo barua rasmi ya kufutwa Kazi ameipata Mei 04 2025 siku jumapili.
Licha ya kumtimua Kali ameifanya Kmc kuwa na matokeo mazuri katika ligi kuu ya soka ya Nbc msimu huu tangu ajiunge nayo miezi michache iliyopita.
Katika msimamo wa ligi kuu nchini mpaka sasa Kmc ina alama 30 katika michezo 26 ya ligi ikiwa katika nafasi ya 11.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kmc inakabiliwa na michezo minne ili kufunga pazia la ligi kuu ya Nbc msimu huu ambapo katika michezo hiyo minne umo mmoja dhidi ya Simba Sc.