Home Soka Simba,Rollers Hakuna Mbabe

Simba,Rollers Hakuna Mbabe

by Dennis Msotwa
0 comments

Timu ya Simba sc imevaana na timu ya Township Rollers ya Botswana katika mechi ya kujiandaa na msimu mpya katika kambi ya maandalizi ya timu hiyo nchini Afrika Kusini na mchezo kuisha kwa sare ya moja moja.

Katika mechi hiyo iliyochezwa saa tano asubuhi kwa saa za Tanzania Simba ilipata goli kupitia kwa Meddie Kagere huku lile la Rollers likifungwa na Serameng huku magoli yote yakipatikana kipindi cha pili.

Simba iliwakosa nyota wake saba ambao wamejiunga na kambi ya timu ya taifa(Taifa stars) kujiandaa na mechi dhidi ya Kenya hapo kesho kutafuta nafasi ya kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani(Chan).

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited