Mshambuliajia Prince Dube kuikosa Derby ya Kariakoo katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC utakaofanyika siku Jumatano Juni 25 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Dube alilazimika kutolewa nje baada ya kuumia kipindi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Juni 18,2025 ambao Yanga sc ilishinda mabao 5-0 Juni 18 2025.
Mratibu wa Yanga Sc Hafidh Saleh alisema mfumania nyavu huyo ataukosa mchezo dhidi ya wapinzani wao wakubwa Simba SC Jumatano baada ya vipimo daktari kubaini kuwa anasumbuliwa na nyama za paja.
“Awali ilikua nyama zimevutika lakini baada ya kujiridhisha kwa Vipimo tumeona kwanza anahitaji muda wa mapumziko mpaka akae sawa hivyo hatocheza siku ya jumatano”.Alisema Hafidh
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc itaivaa Simba Sc katika mchezo ambao inahitaji sare ama ushindi ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini kwa mara ya nne mfululizo.