Home Makala Zahera Ashusha Mashine ya Mabao Usiku

Zahera Ashusha Mashine ya Mabao Usiku

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imempokea Mshambuliaji David Moringa (Falcao) raia wa Kongo kuja kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo jana usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K Nyerere.

Mshambuliaji huyo mwenye mwili mkakamavu aliwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Afisa Habari msaidizi wa klabu hiyo Godlisten Anderson(Chicharito) na kuelekea moja kwa moja hotelini.

Inadaiwa mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Fc Lupopo atasaini mkataba wa miaka miwili na atajiunga na kikosi kilichopo kambini Morogoro hii leo.

banner

Chati ya ufungaji bora ligi ya Congo msimu ulioisha Moringa akishika nafasi ya tano.

Mshambualiaji huyo aliyepachikwa jina la utani Falcao amezichezea klabu kadhaa barani Afrika katika nchi kama Gabon huku akiichezea Club de Augosto na Libolo Clube za Angola huku nchini Kongo akizichezea klabu za Fc Lupopo na Reinassance de Congo.

Falcao ni moja ya wafungaji Bora watano wa Ligi kuu ya Congo msimu uliopita alikamata no 5 kwa kufunga goli 11 huku mfungaji Bora akiwa Muleka toka TP Mazembe akiwa na goli 16.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited