Ni msimu wa mabadiliko ndivyo unavyoweza kusema kutokana na aina ya usajili mpya ambao umefanyika katika klabu ya Azam Fc kwa ajili ya msimu wa ligi kuu na michuano ya kimataifa 2025/2026 ambapo kuanzia ndani ya klabu hiyo unaonekana ni msimu utakaokua na mafanikio katika historia ya timu hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007.
Baada ya kutofanya vizuri kwa takribani misimu kumi sasa ambapo mara ya mwisho walitwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa Huo ndio ulikuwa ubingwa wao wa kwanza na pekee wa ligi kuu hadi sasa.
Katika msimu huo waliotwaa ubingwa Walivunja utawala wa muda mrefu wa Simba SC na Yanga SC kwa kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo wowote msimu mzima (invincible season) wakiwa na Kocha wao wakati huo alikuwa Stewart Hall huku kikosi kilikuwa na nyota kama John Bocco, Salum Abubakar “Sure Boy”, Frank Domayo, na Shomari Kapombe.
Tangu hapo, Azam FC hawajafanikiwa kutwaa tena taji la Ligi Kuu, lakini wamekuwa wakichukua makombe mengine ya ndani kama FA Cup (2019/2020) na Kombe la Mapinduzi mara kadhaa huku msimu huu wakitabiriwa makubwa hasa kutokana na aina ya usajili waliofanya ambao ni ufuatao.
KOCHA FLORENT IBENGE NA BENCHI LAKE LA UFUNDI
Azam Fc ukiingalia aina ya benchi lake la ufundi msimu huu utaona kuwa sasa wameamua kutokua wanyonge tena baada ya kukubali kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kumuajiri mwalimu huyo mzoefu kwa soka la Afrika akiwa amefundisha klabu nyingi kubwa kwa mafanikio zaidi akianza na klabu za ES Wasquehal (Ufaransa) mojawapo ya timu zake za awali akiwa kocha kisha SC Douai (Ufaransa) pia akiwa katika mijiundo yake ya ukocha katika hatua za mwanzo za kazi yake.
Baadaye alijiunga na Shanghai Shenhua (Uchina) ambapo alifundisha kwa kipindi kifupi mnamo Aprili hadi Mei 2012 kisha akajiunga na AS Vita Club (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) ambapo alianza Februari 2014; amefanikiwa kusababisha timu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mataifa ya Afrika (CAF Champions League) 2014. Pia alikuwa na kipindi kirefu na mafanikio ndani ya klabu humo.
Pia Ibenge alijiunga na RS Berkane (Morocco) mnamo Julai 2021, akishinda CAF Confederation Cup mwaka 2022 na pia Kombe la Mwamba (Morocco Throne Cup) kisha akajiunga na Al-Hilal Omdurman (Sudan) kuanzia Juni 2022 hadi mwaka 2025, ambapo alishinda Kombe la Sudan (Sudan Cup).
Kitendo cha kumuajiri Ibenge ambaye amefundisha timu kubwa barani Afrika moja kwa moja kinakwenda kuongeza uzoefu katika levo ya ndani na kimataifa ambapo mara zote klabu hiyo imekua ikitolewa hatua ya mtoani tena mara nyingi zaidi katika hatua ya awali ambapo pamoja na uzoefu wake yeye binafsi pia amekuja na wasaidizi wake Anicet Kiazayidi aliwahi kuwa kocha wa Tabora United,Mehdi Marzouk kutoka Tunisia,Kassim Liogope,Omar Boukathem, Rody Mountaro na Addis Worku.
USAJILI WA FEISAL SALUM
Hii ni sababu nyingine ambayo imekua ni kama usajili mpya baada ya kumshawishi staa huyo kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja na kumfanya sasa awe na miaka miwili zaidi ya kukaa klabuni hapo ambapo sasa staa huyo atatulia na kucheza mpira baada ya kuwa na tetesi nyingi kuhusu kuondoka klabuni hapo hali ambayo kama ingeendelea basi ingeleta ukosefu wa utulivu kutokana na kuandamwa na vyombo vya habari pamoja na viongozi wa timu zinazomnyemelea.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
USAJILI WA WACHEZAJI WA NDANI
Msimu huu Azam Fc imesajili mastaa Aishi Manula,Edward Charles Manyama,Himid Mao,Lameck Lawi,Muhsin Malima,Ally Chamulungu aliyepandishwa kutoka timu ya vijana ya klabu hiyo ambapo usajili huo umelenga kuongeza uzoefu pamoja kuleta ushindani hasa kutokana na kuwapandisha vijana wengi kutoka timu ya vijana jambo ambalo limeleta uendelevu wa kikosi kwa maana wenye umri mkubwa watasaidiwa na vijana wenye nguvu lakini wakikosa uzoefu ambao wataupata kutoka kwa wakongwe kama Himid Mao na Aishi Manula.
Pia kwa kipindi cha misimu miwili sasa klabu hiyo imekua ikisajili wachezaji ambao walipitia katika timu za vijana za klabu hiyo kisha wakaondoka na sasa wanarudishwa kuja kuongeza uzoefu na chachu ya mafanikio baada ya kujifunza kuhusu vilabu vingine ndia maana wakarudishwa wakina Manula,Himid na Muhsin.
USAJILI WA MASTAA WA KIGENI
Azam Fc msimu huu napo imejipanga kwa kusajili mastaa wazoefu wa ligi na michuano ya kimataifa ambapo imewasajili kipa Issa Fofana kutoka Al Hilal Fc ya nchini Sudan ambaye amekua kipa namba moja klabuni hapo kwa muda mrefu lakini pia akiwa kipa namba moja wa timu yake ya Taifa ya Ivory Coast akiungana na Sadio Kanoute aliyewahi kucheza Simba Sc hivyo hana ugeni na ligi kuu nchini akiunga na Japhte Kitambala ambaye yeye moja kwa moja anajuana na Ibenge kwa namna gani atamtumia katika kikosi hicho.
Pia mastaa kama Pape Doudou Diallo ambaye alikua mfungaji bora wa msimu uliopita katika ligi kuu ya Senegal akiungana na wazoefu mshambuliaji mwenye kimo kirefu Ben Zitoun Tayeb pamoja na winga Ihmid Barakat ambao moja kwa moja wanaenda kuleta athari chanya katika kikosi cha timu hiyo hasa eneo la uti wa mgongo huku ujio wa kocha mpya ambaye atakua anaanza upya utaleta chachu ya ushindani zaidi.
Msimu huu kama Azam Fc itashinda michezo yake hasa ya nyumbani dhidi ya timu za Simba Sc,Yanga Sc na Singida Black Stars basi moja kwa moja anaweza kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Nbc.