Home Soka Bigirimana Hali Tete

Bigirimana Hali Tete

by Dennis Msotwa
0 comments

Licha ya kusajiliwa kwa mbwembe na majigambo mengi kwa wanajangwana mpaka sasa Issa Bigirimana hajaonyesha  kile ambacho wanayanga wengi walikitarajia kutoka kwake licha ya kuwahi kuungana na timu mkoani Morogoro katika kambi ya maandalizi ya msimu.

Iko hivi,Sportsleo imebaini sababu kubwa ya staa huyo wa Burundi kutocheza mpaka sasa ni majeraha ya nyama za paja yanayomsumbua kwa muda mrefu tangu akiwa kambini mkoani Morogoro na amekua akipata nafuu japo hajapona kabisa.

Majeraha hayo yamemfanya kiungo mshambuliaji huyo kutoungana na timu mkoani Mwanza katika kambi maalumu ya kujiandaa na mechi ya kimataifa dhidi ya Zesco ya Zambia.

banner

Sportsleo ilifanikiwa kumuona kiungo huyo uwanja wa taifa siku ya mchezo wa Taifa stars dhidi ya Burundi mchezo ambao Taifa stars iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwa penati na baada ya kufatilia kwa undani ndipo lilipobaini taarifa hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited