Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya vijana (Serengeti boys) Kelvin John 17’ leo atapanda ndege kwenda nchini Ubeligiji kusaini mkataba wa kuichezea rasmi timu ya Krc Genk inayoshiriki ligi kuu nchini humo(Jupiler pro).
Kinda huyo ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa(Taifa stars) kilichokwenda nchini Misri kwenye michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon 2019) atajiunga na timu hiyo kama mwanafunzi ambaye anasoma nchini humo huku akiwa anaichezea akademi ya timu hiyo.
Hata hivyo kinda huyo ataanza kazi rasmi mwezi Januari wakati wa usajili wa dirisha dogo barani ulaya na tayari ameshaagwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya vijana.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.