Home Soka Man City Afa kwa Kibonde

Man City Afa kwa Kibonde

by Sports Leo
0 comments

Timu ya soka ya Manchester city chini ya kocha Pep Guardiola imechezea kipigo cha magoli 3-2 dhidi ya Norwich city katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliofanyika katika uwanja wa Carrow Roads.

Makosa binafsi ya mlinzi Nicholaus Otamendi ni moja ya sababu ya kipigo cha city huku Kenny Mclean na Todd Cantwel walifunga mabao ya kutangulia kipindi cha kwanza huku city wakisawazisha kupitia kwa Aguero na Rodri.

Shujaa wa mchezo wa leo ni Teemu Pukki ambaye alipeleka kilio kwa kikosi cha Guardiola baada ya kufunga goli la tatu na kuzoa pointi zote tatu na kuwafanya kushinda mchezo mmoja kati ya mitano waliyocheza hivi karibuni.

banner

Kwa matokeo hayo bado man city wanaendelea kusalia katika nafasi ya pili ya msimamo wakiwa na pointi kumi huku liverpool akiongoza baada ya kushinda michezo yote n kufikisha pointi 15.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited