Home Soka Matic Kumfata Conte

Matic Kumfata Conte

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa klabu ya Manchester United Nemanja Matic yupo mbioni kuachana na klabu hiyo kwenda kujiunga na kocha wake wa zamani Antonio Conte katika klabu ya Inter Milan katika majira ya baridi.

Matic inadaiwa hafurahishwi na jinsi anavyowekwa benchi na kocha Olle Gunnar Solskjaer ambae amewapa kipaumbele kinda Scott Mctominay na Paul Pogba katika eneo la kiungo la timu hiyo.

Kiungo huyo aliyesajiliwa klabuni hapo na Jose Mourinho akiwa ametoka kushinda taji la ligi kuu akiwa chini ya Conte ameanza mara mbili tu katika mechi za ligi kuu msimu huu na yupo katika orodha wa wachezaji wanaowindwa na kocha huyo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited