Home Soka “Siogopi Kufukuzwa”-Zahera

“Siogopi Kufukuzwa”-Zahera

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema haogopi kufukuzwa katika klabu hiyo nan yupo tayari kuondoka endapo uongozi utasitisha mkataba wake unaoisha mwishoni mwa mwaka huu.

Zahera amekua na wakati mgumu klabuni hapo kufuatia matokea mabaya inayopata timu hiyo hasa baada ya kufungwa na Pyramids Fc katika mchezo wa kimataifa iliofanyika jijini Mwanza na kupelekea mashabiki kumrushia chupa za maji.

“Mashabiki ni kawaida yao kuwa wakali siku zote wanataka kuona timu inashinda siku zote kwahiyo sikushanga ile hali”.Alisema Zahera.

banner

Tetesi za kutimuliwa kwa kocha huyo zimezidi kusambaa huku makocha wa zamani waliowahi kuinoa klabu hiyo kama Hans van de pluijm na Erne Brandts wakihusishwa kurejea klabuni hapo pamoja na kocha msaidizi wa klabu ya As vita Raul Shungu na kocha wa zamani wa taifa stars Kim Poulsen.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited