Home Masumbwi Pointi Zambeba Mwakinyo

Pointi Zambeba Mwakinyo

by Sports Leo
0 comments

Bondia Hassan Mwakinyo ameibuka na ushindi mbele ya bondia mfilipino Arnel Tinampay katika pambano la uzito wa juu la raundi 10 lililofanyika uwanja wa uhuru.

Mwakinyo aliyepewa sapoti ya kutosha na watanzania wakiwemo mastaa mbalimbali kama Ommy Dimpoz,Mwana Fa na Ney wa Mitego alishinda kwa pointi za majaji ambao walitoa pointi zifuatazo Jaji wa kwanza ametoa 97 -93 , Jaji wa pili akatoa 98-92 na Jaji wa tatu akatoa 96-96.

“Sijafurahia aina ya ushindi niliuupata ila ni sehemu ya matokeo kwa kuwa ushindani ulikuwa mkubwa na gloves hazikuwa rafiki kwangu, wakati mwingine nitakuwa tofauti zaidi ya hapa,” amesema Mwakinyo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited