Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayeitumikia Klabu ya Difaa El Jadidi inayoshiriki Ligi Kuu ya Nchini Morocco (Batola Pro) Simon Msuva ameendelea Kung’ara baada ya Hapo Kufunga bao Pekee Lililoipa Ushindi Difaa dhidi ya Vinara wa Ligi Hiyo Wydad Casablanca wakiwa Nyumbani katika mchezo wa ligi kuu nchini humo.
Baada ya Ushindi walioupata Difaa wa Bao 1-0 Wanafikisha Alama 16 na kukamata nafasi ya 7 katika Msimamo wa Ligi Hiyo katika michezo 15 waliyoicheza Huku Vinara wa Ligi Hiyo Wydad Casablanca wanaalama 27 katika michezo 16 Walioicheza .
Baada ya kupachika bao la Ushindi katika Mchezo wa Jana Msuva anashika nafasi ya 3 katika orodha ya wafungaji akiwa na mabao 13 Huku kinara wa Orodha Hiyo Mouhcine lajor kutoka Raja Casablanca anamabao 19 akifuatiwa na Kodjo Laba kutoka RSB Berkane mwenye mabao 19
Ikumbukwe Hili Ni bao la tatu Msuva anaifunga Wydad Casablanca katika michuano mbalimbali nchini humo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Credit:Yanga Sports Club