Home Makala Corona imeivusha UEFA Hadi 2021

Corona imeivusha UEFA Hadi 2021

by Sports Leo
0 comments

Kutokana na kuenea kwa Virusi vya Corona ambavyo vilianza kusambaa mwezi Januari,UEFA  wamesitisha michuano ya Euro na inatarajiwa kuanza kufanyika 2021 kati ya Juni 11 mpaka Julai 11 mwaka ujao.

Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin ameamua kusimamisha michuano hiyo msimu huu mpaka msimu ujao ,hii ni baada ya kufanya kikao cha dharura na kamati yake kupitia njia ya simu ya video na kufikia muafaka wa kuhairisha UEFA hadi 2021.

Taarifa iliyotolewa leo na UEFA imeeleza kuwa :” UEFA leo inatangaza kusitisha michuano ya UEFA Euro 2020 kutokana na thamani ya afya za wachezaji na mashabiki kuwa bora kuliko jambo lolote na mpango wetu ni kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima hii ni kutokana na kusambaa kwa kasi Virusi vya Corona”

banner

“Mechi zote za UEFA na mechi za kirafiki,timu za Taifa za Wanawake na Wanaume zinasitishwa mpaka pale tutakapotoa taarifa, mechi zilizotarajiwa kuchezwa mwezi Machi sasa zinaweza kuanza mwezi Juni lakini itategemea na hali itakavyokuwa”

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited