Home Makala Humud Amchomoa Ndemla Yanga Sc

Humud Amchomoa Ndemla Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Jina la kiungo mkabaji wa Mtibwa Sugar, Abdulhalim Humoud ‘Gaucho’ndiyo lililomuondoa Said Ndemla kwenye orodha ya majina ya usajili ya Yanga.

Awali yalikuwepo majina mawili ya viungo wakabaji wazawa  yaliyokuwa yakijadiliwa amabapo moja wapo ni la Ndemla ambaye mkataba wake unakaribia kumeguka mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu Bara.

Humoud ambaye ni nyota wa Mtibwa Sugar ameonekana kuwa na mazungumzo ya siri na kocha mkuu wa Yanga, luc Eymael baada ya kuvutiwa na kiwango chake wakati Yanga ilipocheza mchezo wa Ligi na Mtibwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar-es-salaam.

banner

Nyota huyo alionekana kikwako katika mchezo huwa kutokana na kufanikiwa kupunguza mashambulizi na kuokoa hatari golini kwao.

Ndemla ambaye amekuwa akihusishwa na Yanga mara kwa mara ameondolewa kwenye mipango hiyo ya usajili na Hamoud amepewa nafasi hiyo kama kiungo mkabaji huku Eymal akipanga kumleta mwingine kutoka nje ya nchi.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited