25
Kocha mkuu wa Yanga Sc,Luc Eymael ameweka wazi katika kikosi chake cha msimu ujao hatosajili wachezaji wengi badala yake atafanya maboresho kidogo ya kuchukua wachezaji wachache ambao watakuja kuongeza nguvu kwa waliopo sasa.
Eymael amesema kuwa hatafanya kama ilivyokuwa msimu uliopita wa kocha wa zamani Mwinyi Zahera wa DRC ambapo alisajili zaidi ya wachezaji 11 kwenye dirisha kubwa la usajili.
“Nataka kujenga kikosi imara kwa hiyo sitaweza kusajili namba kubwa ya wachezaji badala yake nitawaboreshea kwenye maeneo kadhaa kisha tutakuwa tayari kupambana,” alisema Eymael