Mechi zilizosalia za ligi kuu Tanzania Bara zitagharimu zaidi ya Sh 417 milioni ambazo zitatumika katika uendeshaji kwa timu na malipo ya posho kwa waamuzi na maofisa wengine wanaosimamia michezo ya Ligi Kuu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa tathmini iliyofanywa na timu ya wataalam wa wizara yake imeonyesha kuwa kiwango hicho cha fedha kinahitajika ili kuweza kumalizia ligi hiyo iliyobakiza raundi 9 (mechi 93).
Waziri amesema kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), klabu pamoja na wadhamini wanalo jukumu la kuona wanamudu vipi gharama hizo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.