Home Soka Molinga,Luc Wawafata Mwadui Kibabe

Molinga,Luc Wawafata Mwadui Kibabe

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa klabu ya Yanga Luc Eymael pamoja na mshambuliaji David Molinga wamepanda ndege kuelekea mjini Shinyanga kuwavaa Mwadui Fc kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaofanyika hapo kesho.

Awali Luc alichelewa kuwasili baada ya kukosa ndege kuja nchini hivyo kuikuta timu ikiwa imetangulia kwa basi wakati Molinga aliachwa baada ya kutokea sintofahamu huku ikielezwa kuwa ana matatizo ya kinidhamu japo mwenyewe alikanusha habari hizo.

Kusafiri kwa wawili hao ni nafuu kwa mashabiki wa Yanga sc kuelekea mchezo huo baada ya timu hiyo kukosa utulivu hasa katika uongozi kutokana na migongano kadhaa inayojitokeza.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited