Home Soka Azam Fc Wakomaa na Yanga

Azam Fc Wakomaa na Yanga

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam fc imeendelea kuipigania nafasi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara baada ya jana kuifunga timu ya Mbao fc mabao 2-0 na kuendelea kusalia nafasi ya pili ya Msimamo.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex,Mabao ya Azam FC yalifungwa na Richard Djod dakika ya 49 kwa pasi ya Idd Naldo huku lile la pili likifungwa na Idd Chilunda dakika ya 90+3.

Mbao baada ya kupoteza mchezo huo unawafanya wasalie nafasi ya 19 ikiwa na pointi zake 23 baada ya kucheza mechi 30 huku Azam wakibaki nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 29.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited