Home Soka Madrid Yaifunga Valencia

Madrid Yaifunga Valencia

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Real Madrid jana iliibuka na ushindi wa magoli 3-0  dhidi ya Valencia katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania (La liga) mchezo uliofanyika katika uwanja wa Alfred Di Stefano ambako mashabiki hawakuhudhuria.

Karimu Benzema alifunga bao zuri dakika ya 61 na aliongeza jingine dakika ya 86 huku Marco Asensio akifunga bao la pili dakika ya 74 huku wageni licha ya kugongesha mwamba wa juu pia walishuhudia staa wao Lee Kang-in akipewa kadi nyekundu dakika ya 89.

Madrid wamefikisha pointi 62 huku Barcelona wakisalia kileleni kwa tofauti ya pointi 2 japo zikiwa zimesalia mechi tisa ligi kumalizika

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited