Kiungo wa klabu ya Manchester United Scott Mctominay amesaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2025 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Kinda huyo mwenye miaka 23 aliyechipukia kutoka akademi ya timu hiyo alianza kupewa nafasi mwaka 2017 na hatimaye kucheza michezo 75 akifunga magoli 6 klabuni hapo.
“Tuna mengi ya kufikiria kipindi hiki lakini nina furaha kusaini mkataba mpya na kutoa mchango mbeleni katika timu hii”Alisema kiungo huyo.