Mchezaji namba 28 aliyetambulishwa na Yanga Sc siku ya wananchi Agosti,31 Benard Morrison sio tena mchezaji wa klabu ya Yanga baada ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) kumtambulisha rasmi kama mchezaji wa Simba Sc.
TFF imetoa uamuzi huo kwa kusimamia maamuzi ya kamati ya Sheria waliyompa Benard Morrison kuchagua timu anayohitaji kuitumikia na yeye akapendekeza Simba Sc kwani mahakama ilimtambulisha Mghana huyo kama mchezaji huru.
Katika usajili mpya wa TFF kwa msimu ujao wa ligi kuu bara jina la Morrison limetokezea Simba Sc hivyo inaonyesha ni mshambuliaji huyo ni mali rasmi ya wanamsimbazi na si wanajangwani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.