Shirikisho la soka Tanzania(TFF) limeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Group Six International wenye thamani ya zaidi ya bilioni 9 kwaajili ya ujenzi wa vituo viwili vya ufundi ‘Techinical centre’ vilivyopo Tanga na Kigamboni.
Vituo hivyo vwili vya ufundi vitakua na viwanja visivyopungua vitatu kwa kila kituo pamoja na hosteli za kisasa ndani yake.
Ujenzi wa miradi hiyo unategemewa kuanza mapema mwezi wa 10, ambapo itajengwa yote kwa pamoja kwa awamu mbili na kutegemewa kumalizika ndani ya kipindi cha miezi 12,kwa maana ya mwaka mmoja.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.