Home Soka Picha Yamponza Aubameyang

Picha Yamponza Aubameyang

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limempiga faini ya USD 10,000 (Tsh milioni 23.1) Nahodha wa Arsenal na Timu ya Taifa ya Gabon Pierre Emerick-Aubameyang kwa kosa la kupost picha inayoishushia hadhi CAF wakati Gabon walipokuwa wamekwama Airport Gambia kwa madai ya kucheleweshwa kwa makusudi na wenyeji wao kama njia ya kuwatoa mchezoni.

Pamoja na hilo Gambia nao wamepigwa faini ya USD 100,000 (Tsh milioni 231.8) na onyo la kutotenda kosa kama hilo kwa kipindi cha miezi 24 la kutowaandalia mapokezi mazuri Wageni wao.

Gambia hawakuwapokea vizuri Gabon wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021 ambapo mwisho wa mchezo Gambia walishinda 2-1.
.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited