Klabu ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Shellfield ugenini katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.
Makosa ya safu ya ulinzi ya Man Utd katika ya kipa na beki Victor Linderlof yalisababisha David McGoldrick kufunga bao la utangulizi kwa wenyeji dakika ya 5 huku akisawazisha dakika ya 26 na dakika saba baadae Athony Martial alifunga goli la pili kabla ya Rashford tena kuongeza goli la tatu dakika ya 51.
David McGoldrick aliipatia Shellfield goli la pili dakika ya 87 na mechi kumalika kwa Man United kupanda mpaka nafasi ya sita wakiwa na alama 23 huku Shellfield wakibaki mkiani na alama moja pekee.