20
Hivi karibuni uongozi wa Simba ulidai kuwa Benard Morrison hakuwa akionekana katika kikosi cha timu hiyo kwa kuwa ni mgonjwa Lakini Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alifichua kuwa mchezaji huyo amepigwa stop na Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS) akisubiri kusikilizwa kwa shauri lake dhidi ya Yanga Januari 12.
Jana katika mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Fc Platnum Morrison alionekana jukwaani wakati timu ya Simba ikicheza na Fc Platinum. Ni tukio lililodhihirisha kauli aliyotoa Mwakalebela baada ya Ismail Aden Rage aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba kudai kuwa uongozi wa Yanga umewahadaa wanachama na mashabiki wake kuwa hakuna kesi waliyofungua CAS

Mwakalebela alisema hatma ya kesi waliyofungua dhidi ya mchezaji huyo itafahamika baada ya kupangiwa Jaji ambaye anaanza kuisikiliza Januari 12.
Ikumbukwe Yanga inapinga hukumu iliyotolewa na kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kubatilisha mkataba wa Morrison na Yanga na kumruhusu mchezaji huyo ajiunge na Simba.
Morrison alipewa nafasi ya kujitetea na CAS lakini utetezi wake ukaonekana hauna mashiko na hivyo kesi hiyo kupangiwa Jaji wa kuisikiliza.
Â
cc.Jacob Mla simba