Home Soka Azam Fc Yatolewa Mapinduzi Cup

Azam Fc Yatolewa Mapinduzi Cup

by Sports Leo
0 comments

Mabingwa wa kihistoria wa kombe la mapinduzi Azam Fc wametolewa katika michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-4 katika changamoto ya matuta baada ya kutoka sare ya 1-1 dakika tisini za mchezo.

Tuisila Kisinda aliwazidi kasi mabeki wa Azam Fc na kufunga bao kwa Yanga sc dakika ya 51 lakini Obrey Chirwa alitumia uzembe wa safu ya ulinzi ya Yanga na kufunga bao dakika ya 67 matokeo ambayo yalidumu mpaka dakika 90 za mchezo.

Katika hatua za penati Michael Sarpong alikosa kwa upande wa Yanga na Awesu Awesu pamoja na Daniel Amoah walikosa penati zao kwa upande wa Azam Fc na kupeleka ushindi jangwani ambao wanasubiri mshindi kati ya Simba sc dhidi ya Namungo Fc ili kucheza fainali.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited