Klabu ya Manchester United imeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kufungwa mabao 2-1 na Shelfield United katika uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza.
Mabao ya Kean Bryan dakika ya 23 na Oliver Burke dakika ya 74 yalitosha kuipa ushindi Shelfied United licha Harry Maguire kusawazisha dakika ya 64 lakini makini mdogo ukisababisha Shelfied kupata bao la pili.
Matokeo hayo yanaifanya Man United kubaki nafasi ya pili na alama 40 huku Man City wakiwa kileleni na alama 41 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.