Klabu ya Yanga sc imepoteza kwa mara ya kwanza mchezo wa Vpl baada ya kukuibali kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union mchezo uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Coastal walipata bao dakika ya 10 kupitia kwa Erick Msagati lakini Tuisila Kisinda alisawazisha dakika ya 35 na kufanya timu kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini uimara wa makipa wa pande zote ulisababisha mchezo ubaki kama ulivyo mpaka dakika ya 85 Mudathir Majimengi alipofunga bao la pili kwa Coastal Union.