Home Soka Mosimane Afunguka Kuivaa Simba sc

Mosimane Afunguka Kuivaa Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa Al Ahly ‘Msauzi’ Pitso Mosimane amesema kutakuwepo na mabadiliko kwenye kikosi chake kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Simba SC.
“Kwa bahati mbaya tuna majerehi kadhaa kikosini hivyo kuna mabadiliko ya lazima ambayo yanatulazimu kuyafanya na kwa hali ya mambo ilivyo wachezaji ambao huwa hawapati nafasi watalazimika kucheza, na ukiangalia mwezi mmoja uliopo mbele yetu una mambo mengi sana ambayo hatupaswa kufanya makosa kwa wachezaji wetu wengi zaidi kupata majeraha” amesema Mosimane kwenye mkutano na waandishi wa habari.
“Nia ya mwanzo ya timu ilikuwa ni kumaliza Kinara wa kundi lakini kwa bahati mbaya hesabu zetu ziliharibika wakati wa mechi yetu na Vita hapa, nisingependa kulizungumzia hilo” aliongeza kocha huyo aliyejizolea sifa barani Afrika.
Mosimane pia ameipongeza Simba kwa kuongoza kundi “Simba sc wamestahili kuwepo hapo ilipo sasa, hakika wamefanya makubwa msimu huu na walijipanga kwa hilo lakini sisi ni Al Ahly, sisi hatuchezi mechi kwaajili ya kisasi, timu yetu ni nzuri”
Cc:Azamtv

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited