Home Soka Lokosa,Muduhwa Wachota Mamilioni Simba sc

Lokosa,Muduhwa Wachota Mamilioni Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Usajili wa mastaa wawili wa klabu ya Simba sc Junior Lokosa na Peter Muduhwa umeigharimu klabu hiyo kiasi cha shilingi milioni 88 ambapo licha ya gharama hizo klabu hiyo imeachana rasmi na wachezaji hao.

Awali taarifa zilisambaa kuwa klabu hiyo imeachana na wachezaji hao iliowasajili kwa ajili ya kucheza michuano ya kimataifa lakini uthibitisho rasmi ulikosekana ambapo kwa mujibu wa gazeti la mwanaspoti sasa ni rasmi suala hilo ni kweli baada ya baadhi ya viongozi kuthibitisha ukweli huo.

Kutokana na kiongozi huyo wachezaji wote wameachwa kutokana na kutokua fiti kwa ajili ya mechi ambapo wanaonekana kutokucheza kwa muda mrefu hasa Lokosa huku kwa upoande wa Muduhwa licha ya kuwa Fiti kiasi alishindwa kuivunja pacha ya Serge Wawa na Joash Onyango.

banner

Taarifa hizo zinadai wachezaji hao walisaini mikataba ya muda mfupi huku wakivuta kiasi cha dola elfu tano kama mshahara lakini hawakupewa fedha ya usajili na wamehudumu klabuni hapo kwa miezi minne tu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited