Home Soka Yanga Yatinga Fainali

Yanga Yatinga Fainali

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara united katika mchezo wa kombe la shirikisho uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mkoani Tabora na kufanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Bao pekee la Yanga sc lilifungwa na Yacouba Sogne dakika ya 22 akipokea pasi kutoka kwa Feisal Salum na kuwahadaa mabeki wa biashara na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa biashara.

Yanga sc sasa itasubiri mshindi kati ya Simba sc dhidi ya Azam Fc mchezo utakaopigwa mjini Songea ili kufahamu timu itakayokutana nayo fainali.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited