Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu Tanzania Almasi Kasongo amesema kuwa ”msimu wa ligi kuu Bara tunatarajia uanze mwezi septemba mwaka huu ingawa mpaka sasa bado hatujapanga tarehe rasmi ya kuanza kwa ligi”.
Hayo yamekuja zikiwa zimepita siku chache tangu kutamatika kwa msimu wa 2020/2021 ambapo klabu ya Simba ilitangazwa na kukabidhiwa ubingwa wa ligi hiyo.Hatua hiyo imeendana pia na kufunguliwa kwa dirisha la usajili kwa wachezaji wa ndani na wale wa kimataifa kuanzia tarehe 19 mwezi Julai.
Kutangazwa kwa hatua hiyo kunaashiria kuwa timu zitakazo shiriki ligi hiyo msimu ujao zina takribani mwezi mmoja wa kupumzika na kuanza maandalizi ya msimu mpya.