Klabu ya soka ya Yanga imewasili tayari Kigoma kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho dhidi ya watani wao wa jadi klabu ya soka ya Simba.
Yanga imetua Kigoma asubuhi ya leo wakiwa na msafara watu 38 wakiwemo wachezaji 20,benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo na kupokelewa na msafara mkubwa wa mashabiki,wanachama na wapenzi wao wa mkoani huo wakiojitokeza kwa wingi kuilaki timu yao.
Yanga watacheza na Simba tarehe 25 Julai katika dimba la Lake Tanganyika katika mchezo wa fainali unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki na wadau wa soka nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.