Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga sc zinasema kwamba klabu hiyo imeachana na beki Lamine Moro kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili.
Awali beki huyo alisaini mkataba wa nyongeza na kubakisha mwaka zaidi kati ya katika mkataba mpya lakini kocha Nasredine Nabi ameonekana kutoridhishwa na nidhamu ya beki huyo hivyo kuamua kuachana nae.
Lamine amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara huku akidaiwa kutoendana na falsafa za kocha mpya kiasi cha kufungiwa mara kwa mara na klabu hiyo.