Home Soka Banda atua Msimbazi

Banda atua Msimbazi

by Sports Leo
0 comments

Winga chipukizi na machachari raia wa Malawi Peter Banda ametua rasmi kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara klabu ya soka ya Simba.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Malawa (20) amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Simba sc hadi mwaka 2024.

Usajili wa mchezaji huyo msimbazi umeondoa sintofahamu ya mashabiki wa soka nchini waliokuwa wana wasiwasi juu ya kinda huyo ni wapi hasa anaelekea kwani ilisemekana ameibwa na wananchi Yanga sc, na anatajwa kuchukua nafasi ya Luis Miquissone anayehusishwa kuelekea Misri katika klabu ya Al Ahly.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited