Beki wa kushoto kutoka klabu ya KMC amejiunga na klabu ya soka ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili kukipiga katika viunga vya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Bryon ni miongoni mwa walinzi wa pembeni wenye uwezo mkubwa katika ligi kuu ya Tanzania Bara anaenda kuongeza ushindani kwenye eneo hilo ndani ya Yanga ambalo tayari lina Adeyun na Yasin Mustapha.
Mchezaji huyo anakuwa ni wa tatu kwa wachezaji wa ndani kusajiliwa Yanga katika dirisha hili baada ya Athuman Yusuph na Dickson Ambundo.