Home Soka Kina Pogba Wapindua Meza Kibabe

Kina Pogba Wapindua Meza Kibabe

by Sports Leo
0 comments

Licha ya kutanguliwa kufungwa mabao 2 na timu ya taifa ya Ubelgiji,Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya Ubelgiji katika mchezo wa ligi ya mataifa ya ulaya uliofanyika jana katika uwanja wa Juventus Stadium nchini Italia.

Mabao mawili ya kipindi cha kwanza ya Yannick Carrasco na Romelo Lukaku yaliwatanguliza wenyeji lakini kipindi cha pili Ufaransa walisawazisha kupitia kwa Karim Benzema na Kylian Mbape huku Theo Hernandez akifunga bao la tatu dakika za mwishoni kwa shuti kali lililomshinda kipa Thabaus Courtous na kuzama wavuni.

Ushindi huo umewapeleka Ufaransa katika hatua ya fainali na watakutana na Hispania ambayo imewafunga Italia huku Italia na Ubelgiji wakitafuta mshindi wa tatu.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited