Home Makala Gsm Ambakisha Mukoko Yanga sc

Gsm Ambakisha Mukoko Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Awali ilielezwa kwamba dili la kiungo Mukoko Tonombe kwenda kujiunga na klabu ya Tp Mazembe ya nchini Congo limekamilika ambapo staa huyo atapishana na winga Chico Ushindi ambaye anakuja Yanga sc lakini mpaka sasa dili hilo limekufa rasmi na mchezaji huyo ameshajiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo jijini Arusha huku kesho akitarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Mbuni Fc ya mkoani humo.

Taarifa za ndani zinadai kuwa dili hilo liligomewa na staa huyo aliyekuwa mchezaji bora wa Yanga sc msimu uliopita ambapo chanzo cha kugoma ni kushindwa kukubaliana maslahi binafsi na timu hiyo huku ikielezwa kwamba Tp Mazembe ilimtaka Mukoko kusaini dili la miaka miwili kwa dau la usajili ambalo staa huyo akiligomea huku akitaka asajiliwe kwa mkopo ili amalizie mkataba wake uliosalia jangwani.

Licha ya kugoma kusafiri kuelekea nchini Congo kukamilisha dili hilo staa huyo pia aliibuka kwa tajiri staa wa timu hiyo Gharib Said Mohamed na kwenda kushtaki ndipo bosi huyo aliamuru kuwa staa huyo arejeshwe kikosini haraka kisha huku akisafirishwa chapchap kujiunga na timu jijini Arusha na akiahidiwa kuwa mazungumzo ya mkataba mpya yataanza muda sio mrefu.

banner

Mukoko amekua hapati nafasi kikosini kutokana na kuwepo kwa mastaa Yanick Bangala na Khalid Aucho ambao wamekua wakianza mara kwa mara kikosini hali ambayo imefanya kukosa raha ikizingatiwa kuwa msimu ulioisha alikua machezaji tegemeo katika kikosi hicho kilichokua chini ya kocha Cedrick Kaze lakini hivi sasa mwalimu Nasredine Nabi anawapanga Aucho na Bangala ama Mauya huku staa huyo akiishia jukwani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited