Home Makala Liverpool Yaipiga Arsenal,Yatinga Fainali

Liverpool Yaipiga Arsenal,Yatinga Fainali

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Arsenal imekubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa kombe la Carabao uliofanyika katika uwanja wa Emirates jijini London ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa awali katika uwanja wa Anfield.

Mabao mawili ya Diogo Jota dakika za 19 na 77 yalitosha kuipeleka Liverpool fainali baada ya kumalizia kazi nzuri za beki Trent-Alexander Anord aliyetoa pasi nzuri za mabao kwa staa huyo.

Mikel Arteta ameingia vinywani mwa wadau wa soka baada ya kumchezesha Thomas Partey ambaye saa chache alikua ametoka kucheza michuano ya Afcon akiwa na taifa lake la Ghana na kusababisha kupata kadi nyekundu dakika 16 tangu aingie uwanjani.

banner

Pamoja na kuwakosa mastaa Sadio Mane na Mo Salah walioko katika michuano ya mataifa ya Afrika Liverpool ilicheza vizuri kiasi cha kupata ushindi huo huku ikitarajia kuvaana na Chelsea katika mchezo wa fainali utakaofanyika katika uwanja wa Wembley jijini London Februari 27.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited