Home Makala Simba sc Yaingilia dili la Mwamnyeto

Simba sc Yaingilia dili la Mwamnyeto

by Dennis Msotwa
0 comments

Ni ubaya ubaya tu..ndivyo tunaweza kusema baada ya klabu ya Simba sc kuanza mazungumzo ya kumsajili beki kisiki wa klabu ya Yanga sc na timu ya Taifa Bakari Mwamnyeto ambaye mkataba wake umbakisha miezi mitani katika klabu ayke ya Yanga sc.

Inasemekana huku tayari Yanga sc na beki huyo mazungumzo yamefikia asilimia 98 kuhusu kusaini mkataba mpya na wameshakubaliana vitu vya msingi huku vikibaki vichache tu lakini kuingia kwa Simba sc katika dili hilo kunaweza kubadili hali ya mchezo na beki huyo akatua upande wa pili kutokana na ushawishi wa fedha alionao bilionea wa klabu hiyo Mohamed Dewji.

Simba sc misimu miwili iliyopita ilimkosa beki huyo baada ya vita kali ya usajili ambapo Yanga sc walifanikiwa kumsajili kwa dau linalosemekana kufikia kiasi cha Tsh 230 ambapo katika dau hilo shilingi milioni 150 zilikua za kuvunja mkataba katika klabu ya Coastal Union.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited