Taarifa kutoka nchini Morocco zinasema kuwa endapo kocha wa RS Berkane, Florent Ibenge ambaye ni Raia wa Congo endapo atashindwa kuifunga Simba atafukuzwa kuwa kocha wa klabu hiyo katika mchezo wa marudiano Jumapili kwenye uwanja wa Mkapa katika kombe la Shirikisho Afrika.
Ibenge alijiuga na Rs Berkane mwezi Julai mwaka jana akitokea klabu ya As Vita ya nchini Congo alipofundisha kwa miaka tisa anakabiriwa na kibarua kigumu kuwashawishi mabosi wa klabu hiyo kumbakiza klabuni hapo huku mechi hiyo dhidi ya Simba sc ikiwa ni mtego kwake ambapo akipoteza basi anaweza kutimuliwa.
Rs Berkane chini ya Ibenge imekua na mwendo wa kusuasua ambapo katika michezo 23 ya hivi karibuni imeshinda michezo nane pekee na kutoa sare michezo kumi huku ikifungwa katika michezo mitano.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.