Home Makala 250m Kumpata Yakoub wa Jkt Tanzania

250m Kumpata Yakoub wa Jkt Tanzania

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Jkt Tanzania inahitaji kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni 250 ikiwa ni ada ya usajili ili kumuachia golikipa wao Yakoub Suleiman (25) ambaye anatakiwa na klabu ya Simba Sc msimu ujao.

Simba Sc tayari imewasiliana na JKT Tanzania ikitaka saini ya kipa huyo ambaye alikuwa na msimu bora akimaliza na clean sheet nane katika ligi kuu msimu huu na mazungumzo yameanza baina ya timu hizo.

banner

Simba sc inahitaji sana huduma ya golikipa huyo kuelekea msimu ujao kwa ajili ya kutoa ushindani kwa Moussa Camara na tayari imempoteza kipa Aishi Manula aliyejiunga na Azam Fc na sasa mchakato umeanza na mazungumzo yanaendelea vizuri sana baina ya pande zote mbili

Simba sc itaachana na kipa Hussein Abel ambaye ameshindwa kuwashawishi mabosi wa klabu hiyo na sasa inaingia sokoni kumsaka mrithi wake.

Kwenye mechi 21 za ligi kuu akiwa na JKT,Yakubu Suleimani ameweza kuondoka na clean sheets 8,alikuwa na msimu mzuri mpaka ikamfanya aitwe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars”.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited