Klabu ya Simba sc ipo katika mipango mikali ya kusuka kikosi cha msimi ujao ambapo baada ya kumaliza msimu wakiwa katika nafasi ya pili wataachana na Kipa Hussein Abel kutokana na uwezo wake kutoridhisha tangu amejiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu ulioisha.
Mabosi wa Simba wapo katika mchakato wa kutafuta kipa mwingine ambae atakuja kuziba nafasi ya kipa huyo msimu ujao na taarifa za awali zinaripoti kuwa wapo katika hatua nzuri za kunasa saini ya Kipa wa JKT Tanzania.
Abel alijiunga na Simba Sc akitokea klabu ya Tanzania prisons ya jijini Mbeya na wakati huu kuna vilabu kadha ambavyo vimeanza kuonyesha nia ya kuhitaji saini yake kwa ajili ya msimu ujao.